Simba yashindwa kesi Fifa.. Yapigwa faini. Soma hapa
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), jana Alhamis asubuhi lilitoa hukumu ya kesi ya beki wa zamani wa Simba, Mkenya Donald Mosoti na kuamuru klabu hiyo ya Msimbazi kumlipa beki huyo Dola 14,000 (Sh24 milioni) kutokana na kuvunja mkataba wake.
Hiyo ni kesi ya kwanza kwa uongozi wa sasa wa Simba, chini ya Rais Evans Aveva kushindwa ingawa bado hawajapewa taarifa rasmi.
Fifa imeitaka Simba kumlipa Mosoti ndani ya siku
21 tangu hukumu hiyo ilipotolewa jana. Mosoti alifungua kesi hiyo
kupitia Wakili wake Felix Majani ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa
shirikisho hilo la kimataifa.
Simba ilikata jina Mosoti katika usajili wa msimu
huu wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni siku chache kabla ya dirisha kufungwa,
nafasi ya Mosoti ikajazwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi. Mosoti
alibakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Kabla ya kuanza kusikiliza kesi hiyo mwaka jana,
Fifa iliwataka Simba kupeleka vielelezo vya mikataba ya mchezaji huyo
kama utetezi wao, lakini ilishindwa kufanya hivyo na kesi ilisikilizwa
kwa vielelezo vya upande mmoja na kutolewa hukumu.
Wakati kesi inaendelea, Fifa ilimruhusu Mosoti
kutafuta timu nyingine ili kulinda kiwango chake ma alisajiliwa na
Tusker FC ya Kenya.
Post a Comment