Phiri VS Waganda



Wakati Simba leo ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe leo, kKkocha Patrick Phiri amesema kuchelewa kwa nyota wake watatu Waganda kunatibua mipango yake.Hadi jana mchana Juuko Murshid, Simon Sserunkuma na Emmanuel Okwi walikuwa hawajafika kambini.
Phiri alisema endapo wachezaji hao watachelewa zaidi, atashindwa kuwatumia katika mechi ijayo ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.
“Labda jioni (jana jioni) ndiyo wataingia lakiniila walitakiwa wafike tangu jana (juzi). K, kwa upande wa Okwi sababu yake inaeleweka ila anapaswa kufika mapema kwani
nimemwambia arudi kabla ya mechi hiyo,” alisema Phiri.
Akizungumzia mechi yake dhidi ya Taifa Jang’ombe, Mzambia huyo alimesema atatumia mechi hiyo kutengeneza kombinesheni ya kikosi chache pamoja na kuwapa nafasi zaidi Mganda Dan Sserunkuma na beki Hassan Kessy.
Phiri alisema Sserunkuma na Kessy hawajapata mechi nyingi za majaribio hivyo atawachezesha kwa dakika 90 ili kuona ni jinsi gani wataingia katika kikosi chake.
“Ukiangalia nafasi anayocheza Kessy yupo Nassoro Masoud ‘Chollo’, Willam Lucian ‘Gallas’ wote ni wazuri, naamini hadi mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar nitajua nani anaweza kuanza,” alisema Phiri.
“Unajua Simba kwa sasa imeimarika zaidi sijui nimtumie mchezaji gani na yupi nimwuache, inanipa wakati mgumu, lakini nitaangalia mwenye kujituma zaidi ndiye atakayepata nafasi, mechi hiyo itanipa mwanga zaidi wa jinsi ya kuwatumia wachezaji hao maana siwezi kusema watakwenda moja kwa moja katika kikosi cha kwanza.”
Simba ipo kambini Zanzibar na, inatarajia kurejea jijini Dar es Salaam kesho mchana tayari kwa mechi yake ya raundi ya nane dhidi ya Kagera Sugar.

No comments