KOCHA mkuu wa Express ya Uganda, Wasswa Bbossa, ameishtua beki ya Yanga kuwa makini na wachezaji wa Simba, Dan Sserunkuma na Emmanuel Okwi ambao watatengeneza kombinesheni moja kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe.
Bbossa ambaye alikuja nchini pamoja na kikosi cha Express kilichocheza dhidi ya Simba na Yanga wikiendi iliyopita, amesema anajua beki ya Wanajangwani hao iliyo chini ya nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani ‘Vidic’ ni nzuri lakini Okwi na Sserunkuma ni wasumbufu mno.
Akizungumza na Mwanaspoti, Bbossa alisema: “Ninawajua wachezaji hao, Okwi na Sserunkuma wote wana kasi, hawaogopi na wana nguvu kama watapangwa kwa pamoja siku hiyo ni hatari, watawasumbua sana beki wa Yanga.Mfano Sserunkuma ni mchezaji ambaye namjua vizuri, tulikuwa naye kabla ya kwenda Gor Mahia naweza kusema ni namba moja kwenye kufunga mabao kwa Uganda.
“Ni mchezaji ambaye anatamani kufunga wakati wote kila anapolikaribia goli na mara chache sana anakosa, kwa kweli Simba imefanya jambo la maana sana kumsajili. Okwi naye ni mfungaji mzuri.”
Akizungumzia uwezo wa wachezaji hao, Bbossa aliongeza: “Wote ni wachezaji wazuri wana kasi na nguvu, Sserunkuma ni mchezaji ambaye ana hamu ya kufunga muda wote anapolikaribia goli, yaani anapenda kufunga ni hivyo pia kwa Okwi.
“Simba na Yanga ni timu ambazo zinacheza kitimu na hawajaonyesha papara katika mechi tulizocheza nao, lakini jambo kubwa kutokana na ukongwe wao wanatakiwa waimarishe safu zao ushambuliaji.”
Post a Comment