Katibu mkuu Yanga kupitia upya anza na mikataba ya udhamini


Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Dk. Jonas Tiboroha akizungumza na waandishi wa habari ,Dar es Salaam jana kulia ni Mkurugenzi wa habari wa Yanga, Jerry Muro

Katibu mpya wa Yanga, Dk .Jonas Tiboroha ametangaza mikakati yake ya kuhakikisha klabu hiyo inajiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupitia upya mikataba yote ya wadhamini.
Akizungumza kwenye mMakao mMakuu ya klabu hiyo jana, Tiboraha alisema kuwa Yanga ni klabu kubwa, inatakiwa kujiendesha yenyewebadala ya kutegemea mtu binafsi na kwamba haiwezi kuwa na mikataba ambayo haikidthi masilahi ya klabu hiyo.
“Yanga ni bidhaa inayojiunza yenyewe, huwezi kuingia mkataba wake sawa na Stand United. H, haiwezekani ikapata mgawo sawa kama wanafunzi wa shule ya msingi unawapanga mstari unawaambia haya kila mtu unamgawia pipi moja moja na wanaridhika, haiwezekani ni lazima Yanga iwe tofauti.
“Klabu kama Liverpool, ina mwashabiki wengi hata kama haipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi, linapokuja suala la mgawo wa fedha, inapata fungu kubwa kwa vile tayari inajiuza, sasa Yanga iingie mikataba sawa na kina Stand United dunia nzima itatushangaa,.” alisema.
Alisema sekretartrieti mpya ambayo wanaiongoza ipo kwenye mchakato wa kupitia upya mikataba ya TBL, Vodacom na Azam ambayo hadi sasa klabu hiyo ya Jangwani imesusia fedha zake iwakidai nyongeza kwa vile haiwawezi pata mgawo sawa na timu nyingine.
Hata hivyo, haki za televisheni ni mali ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati mikataba ya udhamini inatakiwa isainiwe kutokana na utashi wa klabu nyingi za Ligi Kuu.
Hata hivyo, Tiboraha, ambaye ni mhadhiri wanafalsafa wa mMichezo wa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema mpira wa Tanzania umegubikwa na changamoto kubwa na kwamba miezi minne aliyofanya kazi TFF, amegundua Yanga kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili iweze kutoka hapo ilipo na kusonga mbele.
Katika hatua nyingine, Tiboraha alisema hana wasiwasi na kutimuliwa Yanga iwapo uwezo wake utaonekana mdogo kutokana na rekodi ya uongozi katikahistoria ya mklabu hiyo ambayo ndani ya miaka miwili ya kutimua watendaji.

No comments