Wayne Rooney aipa Man U ushindi na aweka rekodi hii mpya
Manchester United jana imepata ushindi wa kwanza ugenini kwenye ligi kuu ya England msimu huu baada ya kuifunga Arsenal 2-1 kwenye uwanja wao wa Emirates, jijini London.
Kieran Gibbs alianza kwa kujifunga kabla ya nahodha wa England na Manchester United Wayne Rooney kufunga goli la pili na la ushindi kwa timu yake.
Goli hilo limemfanya Wayne Rooney kuwa ndio mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi klabu ya Arsenal – magoli 11.
Kwa maana hiyo Rooney amempita mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na England Robbie Fowler ambaye ndio alikuwa anaongoza kwa kuifunga Gunners – magoli 10.
Rooney alianza kuifunga Arsenal katika mechi yake ya kwanza kabisa ya ligi kuu ya England -wakati akiwa na miaka 16 alipokuwa akiichezea klabu ya Everton.
Goli la Rooney la leo limeifanya Arsenal kupoteza mechi yao ya kwanza kwenye uwanja wao wa Emirates msimu katika EPL
Post a Comment