Najitokeza katika safu hizi kuhitaji msaada katika hili; Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23,nilitokea kumpenda sana binti mmoja jina lake (....) naye akakubaliana nami ,tukapendana sana tena kwa dhati.Siku hadi siku shida na matatizo yake yote nilimtatulia.
Basi akaona isiwe tatizo, akaniambia mimi nimekupenda sana na naona thamani na furaha kuishi nawe katika hii dunia na hata ahera hivyo naomba nikakutambulishe nyumbani kwa baba na mama na ndugu zangu wakufaham.
Kwakua nilimpenda hata zaidi yake nikaona hii ni baraka na bahati ya pekee na wala nisikawie kukubali huenda akabadili mawazo.Nikamueleza basi jitahidi iwe ndani ya siku hizi mbili kwani huenda nikasafiri kikazi baada ya siku mbili zijazo.Kiukweli sikuwa na safari bali nilihitaji nisije nikachelewa akabadili mtazamo.
Basi kama nilivyo mueleza akatekeleza na siku ya pili tukaenda kwao,baba na mama yake walifurahi kuniona pia na ndugu zake,.Baba akanieleza nashukuru kumuona binti yangu na kumpenda,jitahidi baada ya miaka miwili kumlea liwe jukumu lako, kwani wakati huo alikuwa akisoma chuo kimoja jijini Dar - Posta cha usimamizi wa fedha.
Kwakuwa nilikuwa tayari nina kazi sikuona tatizo nikamueleza baba hili sitatizo kwangu na nimefurahi sana kusikia hivyo nakuahidi mimi nitampenda na kwamwe sitothubutu kumuacha na zaidi baba kwa miaka hii miwili iliyobaki mimi nitamsomesha.Baba na mama yake walifurahi sana kusikia hivyo.
Basi sikukawia kuanza majukumu yangu,nilimsomesha na shida zake zote nilimtatulia tena kwa wakati.Muda wote huo hatujawahi kuingia katika mahusino ya kimapenzi kwani yeye alikuwa wadini nami vilevile.
Leo amakweli najikuta nikitoa machozi kama mtoto,binti kamaliza chuo MUNGU kamsiidia nimemtafutia kazi na amepata. Sasa ananieleza
"Mama yangu ameniambia mimi siwezi ishi na wewe,nami nimeona kweli huwezi ishi na mimi naomba utafute mchumba mwingine mimi tayari nina mchumba na wala sikutaki tena."
Nilitamani dunia ipasuke niingie lakini...,kweli inaniuma,mimi fedha zote nilizo msomesha na kumsaidia sijali bali muda niliopoteza kumsubiri ndio kidonda ndugu kwangu huenda angenieleza mapema leo ningekuwa hata na mtoto mmoja. Kwa upande wa baba yake yeye binafsi anaonesha kutoafikiana na mtazamo wa binti na mamaye lakini ndio hana sauti mbele yao.
Sifahamu hata tatizo ni nini ama kwakuwa nimesimamishwa kazi,sielewi,ama huyo aliye mpata ana hela sana sifaham,ama.... nabaki na mtindio wa mawazo.....
Wana MF naomba msaada wenu katika hili, kwani limechukua nafasi kubwa ya akili yangu na hata ufanisi wangu wa kazi umeathiriwa kwa kiasi kikubwa , wakati mwingine nafikia hatua ya kukata tamaa,lakini kamwe sito kata tamaa lakin sifahamu hata kama yatapita haya!!!! Msaada tafadhali.
Post a Comment