Jamaa aligombana na mkewe akasusa kula. Aliporudi kazini akamkuta mkewe kavaa khanga imeandikwa "UKISUSA WENZIO WALA." Ilipofika asubuhi mkewe akavaa khanga imeandikwa "UKITOKA MWENZIO ANAINGIA." Jamaa kuona hivyo akagoma kwenda kazini.

Mwanamke kuona hivyo akavaa khanga iliyoandikwa "HAMNIWEZI NIMEMDHIBITI NDIYOMAANA HATOKI." Jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake, rafiki yake akamwambia twende huko kwa mkeo tukayazungumze tuyamalize. Walipofika nyumbani walimkuta mwanamke amevaa khanga imeandikwa "ULIDHANI RAFIKI KUMBE ADUI YAKO."

Hapama chezea khanga za India wewe!