Najitokeza katika safu hizi za MF kuhitaji msaada katika hili;
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23,nilitokea kumpenda sana binti
mmoja jina lake (....) naye akakubaliana nami ,tukapendana sana tena kwa
dhati.Siku hadi siku shida na matatizo yake yote nilimtatulia.
Basi akaona isiwe tatizo, akaniambia mimi nimekupenda sana na naona
thamani na furaha kuishi nawe katika hii dunia na hata ahera hivyo
naomba nikakutambulishe nyumbani kwa baba na mama na ndugu zangu
wakufaham.
Kwakua nilimpenda hata zaidi yake nikaona hii ni baraka na bahati ya
pekee na wala nisikawie kukubali huenda akabadili mawazo.Nikamueleza
basi jitahidi iwe ndani ya siku hizi mbili kwani huenda nikasafiri
kikazi baada ya siku mbili zijazo.Kiukweli sikuwa na safari bali
nilihitaji nisije nikachelewa akabadili mtazamo.
Basi kama nilivyo mueleza akatekeleza na siku ya pili tukaenda kwao,baba
na mama yake walifurahi kuniona pia na ndugu zake,.Baba akanieleza
nashukuru kumuona binti yangu na kumpenda,jitahidi baada ya miaka miwili
kumlea liwe jukumu lako, kwani wakati huo alikuwa akisoma chuo kimoja
jijini Dar - Posta cha usimamizi wa fedha.
Kwakuwa nilikuwa tayari nina kazi sikuona tatizo nikamueleza baba hili
sitatizo kwangu na nimefurahi sana kusikia hivyo nakuahidi mimi
nitampenda na kwamwe sitothubutu kumuacha na zaidi baba kwa miaka hii
miwili iliyobaki mimi nitamsomesha.Baba na mama yake walifurahi sana
kusikia hivyo.
Basi sikukawia kuanza majukumu yangu,nilimsomesha na shida zake zote
nilimtatulia tena kwa wakati.Muda wote huo hatujawahi kuingia katika
mahusino ya kimapenzi kwani yeye alikuwa wadini nami vilevile.
Leo amakweli najikuta nikitoa machozi kama mtoto,binti kamaliza chuo MUNGU kamsiidia nimemtafutia kazi na amepata.
Sasa ananieleza "Mama
yangu ameniambia mimi siwezi ishi na wewe,nami nimeona kweli huwezi
ishi na mimi naomba utafute mchumba mwingine mimi tayari nina mchumba na
wala sikutaki tena."
Nilitamani dunia ipasuke niingie lakini...,kweli inaniuma,mimi fedha
zote nilizo msomesha na kumsaidia sijali bali muda niliopoteza kumsubiri
ndio kidonda ndugu kwangu huenda angenieleza mapema leo ningekuwa hata
na mtoto mmoja.
Kwa upande wa baba yake yeye binafsi anaonesha kutoafikiana na mtazamo wa binti na mamaye lakini ndio hana sauti mbele yao.
Sifahamu hata tatizo ni nini ama kwakuwa nimesimamishwa kazi,sielewi,ama huyo aliye mpata ana hela sana sifaham,ama....
nabaki na mtindio wa mawazo.....
Wana MF naomba msaada wenu katika hili, kwani limechukua nafasi kubwa ya
akili yangu na hata ufanisi wangu wa kazi umeathiriwa kwa kiasi kikubwa
, wakati mwingine nafikia hatua ya kukata tamaa,lakini kamwe sito kata
tamaa lakin sifahamu hata kama yatapita haya!!!!
Msaada tafadhali
Post a Comment