Aliyemsulubu mtoto aburuzwa mahakamani

TEDDY Omary John ( 22 ) , mkazi wa Tegeta
jijini Dar amejikuta akihenyeshwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa
tuhuma za kumchoma na kumjeruhi mtoto
Magdalena Elisha ( 10) na kitu chenye ncha
kali mapajani na kumsababishia maumivu
makali.
Teddy Omary John ( 22 ) , mkazi wa Tegeta
jijini Dar anayetuhumiwa kumsulubu mtoto ,
Magdalena Elisha .
Imedaiwa kuwa , mtuhumiwa ambaye alikuwa
akiishi na binti huyo kama mfanyakazi wake
wa ndani ( hausigeli ) , kwa sababu ambazo
hazikufahamika alimchoma na kitu chenye
ncha kali Magdalena pamoja na kumchoma
na mshumaa.
Akisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu A.
Kupa ambalo alidaiwa kulitenda huku akijua
ni kinyume cha sheria, Mwendesha Mashtaka
S. Magoma alisema kuwa Julai 30, mwaka
huu– maeneo ya Mbezi - Beach mtuhumiwa
alimjeruhi mtoto huyo na kitu chenye ncha
kali na kumsababishia maumivu makali.
Katika kesi hiyo , Teddy alipokuwa akihojiwa,
aliyakana mashtaka ya msingi ambapo
mahojiano baina ya hakimu na mtuhumiwa
yalikuwa hivi :
Teddy Omary John akiwa mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni .
Hakimu: Wewe ni mkazi wa Tegeta ?
Teddy: Ndiyo.
Hakimu: Mnamo tarehe 30 , Julai ulikuwa
Mbezi Beach jijini Dar ?
Teddy: Ndiyo.
Hakimu: Bila uhalali ulimchoma na
kumkwaruza Magdalena Elisha na kitu
chenye ncha kali ?
Teddy: Si kweli .
Mtuhumiwa Teddy akirudishwa kizimbani
chini ya ulinzi mkali.
Hakimu: Kwa mara ya kwanza ulipokamatwa
na kuhojiwa na polisi ulikiri kosa lako ?
Teddy: Si kweli .
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 22,
mwaka huu itakaposikilizwa tena katika
mahakama hiyo na mtuhumiwa alirudishwa
kizimbani kusubiri taratibu za dhamana
ambayo ilikuwa wazi.

No comments