Kipindi cha kwanza ilikuwa nipe nikupe kati ya vijana wa Mourinho na mabingwa msimu uliopita wa ligi ya daraja la pili.
Hata hivyo hakuna yeyote aliyewahi kufunga mwenzake bao katika kipindi cha kwanza.Kipa mgeni Stamford Bridge Thibaut Courtois alifanya kazi ya ziada na kudhihirisha kwanini mkufunzi Jose Mourinho alimteua kuanza langoni badala yake kipa Petr Cech.
Hata hivyo katika kipindi cha pili ni mshambulizi huyo kutoka Uhispania aliyetokea Atletico Madrid aliyecheka na wavu na kuibua shangwe uwanjani Stamford Bridge.
Hazard aliifungia Chelsea bao la pili.
Costa alitumia pasi safi ya Branislav Ivanović katika eneo la lango na kutikisa wavu kunako dakika ya 63 ya kipindi cha pili.
Leicester walijifurukuta na kufanya mashambulizi dhidi ya Chelsea lakini utepetevu wa mshambulizi wao wa kutegemewa David Nugent
uliwanyima fursa hiyo ya kipekee.
Vijana wa Mourinho waliendeleza mashambulizi hayo na juhudi zao zikazawadiwa kunako dakika ya 77 Eden Hazard alipofuma mkwaju kimiani na kumwacha kipa Kaspar Schmeichel asijue iliipitia wapi.
Bao hilo linamaanisha Chelsea wamesajili ushindi wao wa pili katika mechi yao ya pili msimu huu.
Katika matokeo mengine ya leo Aston Villa ilitoka sare tasa na Newcastle
West Ham ikaiadhibu vikali Crystal Palace mabao 1 - 3 .
Southampton walitoka sare tasa na West Brom huku Swansea ikiendeleza msururu wa matokeo mema kwa kuibana
Burnley 1-0
Post a Comment