
BENCHI la Ufundi la Yanga lilifanya uteuzi wa kumpa beki Mbuyu Twite nafasi ya unahodha kuchukua nafasi ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mchezo dhidi ya Azam FC Jumapili, lakini Twite akagoma akisema: “Kiswahili yangu haipo sawa!”
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Azam na Yanga zilitoka sare ya mabao 2-2 na baada ya Twite kukataa cheo hicho, Haruna Niyonzima alichukua jukumu hilo na kazi ikaendelea.
Akizungumza na Mwanaspoti, Twite alisema: “Nilitakiwa kuwa nahodha katika mchezo huo lakini niliomba wampe mtu mwingine kwani lafudhi yangu ya lugha ya Kiswahili haipo sawa.
“Ile ni mechi kubwa sana ningekuwa nahitajika kuwasiliana na mwamuzi kila baada ya muda katika kuitetea timu yangu, sasa kiswahili yangu siyo nzuri ingenipa shida,” alisema Twite.
“Niliomba wanibadilishe ndiyo maana akapewa Haruna, sote tulikubaliana na hilo, Ninaweza kuwa nahodha Yanga katika mechi nyingine ndogo lakini siyo kubwa kama hile.”
Post a Comment