Rekodi za Yanga kwenye michuano ya kombe la Kagame
Yanga inaingia kwenye michuano hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kushika nafasi ya pili kwa kutwaa ubingwa huo mara tano nyuma ya wapinzani wake wa jadi Simba
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame Yanga tayari wameingia kambini kujiandaa na michuano iliyopangwa kuanza Julai 18 kwenye viwanja wa Karume na Taifa Dar es Salaam.
Wanafanana na Gor Mahia
Yanga inaingia kwenye michuano hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kushika nafasi ya pili kwa kutwaa ubingwa huo mara tano nyuma ya wapinzani wake wa jadi kwenye soka la Tanzania bara Simba ambao wamechukua ubingwa huo mara sita.
Klabu kongwe ya Gor Mahia ya Kenya ambayo imepangwa kundi moja na Yanga kwenye michuano ya mwaka huu nayo ipo sawa na wawakilishi hao wa Tanzania kwa kunyakua ubingwa huo mara tano.
Tofauti ya Yanga na Gor Mahia ni kwamba vijana hao wa kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, ni kuchukua ubingwa huo mara nyingi ikiwa nje ya ardhi ya nyumbani mara mbili ikiwa Uganda na timu moja ya Sports Club Villa.
Klabu hiyo inayoongoza kwa kutwaa mara nyingi taji la Ligi Kuu hapa nchini, ni miongoni mwa timu ambazo zimefanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na kusimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Ubingwa wa Kwanza
Ubingwa wa Kwanza
Ilianza kuweka rekodi ya kutwa ubingwa wa michuano hiyo ambayo unafanyika kwa mwaka 40 mwaka huu mwaka 1975 ambapo mwaka hui ilitinga fainali na Simba kwenye uwanja wa Uhuru wakati huo ukiitwa uwanja wa taifa na kushinda mabao 2-0.
Mwaka 1976 Yanga ilikaribia kutetea ubingwa wake baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo lakini ikajikuta ikifungwa na Luo Union ya Kenya kwa mabao 2-1 kupokonywa taji hilo.
Baada ya kukosa taji hilo Yanga ilipotea kabisa kwenye michuano hiyo na mara kadhaa ilijikuta ikitolewa kwenye hatua za awali hadi mwaka 1993 ilipoweza kuchukua ubingwa huo kwa mara ya pili baada ya kuwafunga Sports Club Villa ya Uganda mabao 2-1 kwenye uwanja na Nakivubo.
Yanga ikaweza kurudia rekodi yake kwa mara ya pili kwenye uwanja huohuo na timu hiyo hiyo ya Villa kwa kuifunga kwenye fainali ya mwaka 1999 ikiwa ni miaka sita imepita baada ya kutoka sare katika dakika 90 Yanga wakashinda kwa mikwaju ya penalty.
Wagomea Mechi
Wagomea Mechi
Baaada ya kimya kirefu wawakilishi hao wa Tanzania wakaonekana kupotea tena kwenye michuano hiyo kabla ya kuibuka na kasi mpya tena wakitokea kwenye kifungo cha miaka mitatu baada ya kugomea kucheza mechi ya mshindi wa tatu mwaka 2008 dhidi ya mpinzani wake Simba.
Na mara walipomaliza adhabu na kurudishwa kwenye michuano hiyo mwaka 2011 Yanga ikafanya kwenye kwa kunyakua ubingwa huo kwa mara ya nne safari hii ikiwafunga ndugu zao Simba kwa bao 1-0 mchezo ukifanyika uwanja mpya wa taifa na mfungaji wa bao hilo akiwa Keneth Asomoah raia wa Ghana.
Mwaka uliofuta vijana hao wa Jangwani safari hii wakiwa chini ya kocha Mbelgiji Tom Saintfit waliweza kutetea ubingwa wao wakiwa tena nyumbani safari hii wakiwafunga ndugu zao Azam FC, mabao 2-0 mabao hayo yakifungwa na Mganda Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi.
Waikaribia rekodi ya Simba
Waikaribia rekodi ya Simba
Kukosekana kwa Simba kwenye michuano ya mwaka huu kunazipa nafasi Yanga na Gor Mahia kuweza kuifikia Simba ambayo ndiyo bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1967.
Timu hizo mbili zilizo twaa ubingwa huo mara tano zimepangwa kundi moja na ndizo zitakazo cheza mechi ya ufunguzi Jumamosi lakini pamoja na kuwepo kundi moja Yanga ndiyo inayopewa nafasi kubwa kwasababu katika mara tano iliweza kuchukua ubingwa huo mara tatu imefanya hivyo ikiwa kwenye aridhi na timu za nyumbani mara mbili ikiwa Simba na mara moja Azam.
Lakini sababu nyingine ya Yanga kupewa nafasi ni ubora wa kikosi ilihokuwa nacho wakati huu ukilinganisha na kile cha Gor Mahia ambacho hakina nyota wengi wakali kama ilivyokuwa msimu uliopita licha ya kwamba timu zote mbili ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu za nchi zao Tanzania na Kenya kwa msimu uliopita.
Post a Comment