Twiga stars yafanya kweli... Inastahili pongezi kwa hili
Twiga Stars’ l imefanikiwa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zitakazi fanyika Congo Brazavile mwezi Septemba
LICHA ya kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Zambia ‘She-Polopolo’ timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ leo imefanikiwa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zitakazi fanyika Congo Brazivile mwezi Septemba kwa jumla ya mabao 6-5.
Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogacian Kaijage ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 lakini kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwao baada ya kocha wa Zambia She Polopolo Albert Kachinga, kuusoma mchezo na kubadili mbinu ambazo ziliweza kuwasaidia kupata ushindi huo japo haukuwasaidia kusonga mbele.
Matumaini ya Watanzania kuiona timu yao ya‘Twiga Stars’ kuibuka na ushindi lianza kuonekaa dakika ya pili ya mchezo baada ya Asha Rashid kufunga bao kwa shuti kali akiwa pembeni karibu na kibendera cha kupigia kona na Mwanahasi Omari akafunga bao la pili dakika ya 28 akimalizia makosa ya mabeki wa Zambia walioshindwa kuondosha mpira wa kurusha.
Lakini kipindi cha pili Zambia walikuja kivingine na kuliandama mfululizo lango la ‘Twiga na kufanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Grace Chanda dakika ya 50 akimalizia krosi ya Barbra Banda.
Bao hilo lilionekana kuwapanga nguvu She- Polo polo na kuendelea kuliandama lango la Twiga na dakika ya 54 Misoz Chisa Rachel, alipoteza nafasi ya wazi kufuatia shuti lake kudakwa na kipa Fatuma Omar wa Twiga.
Mabadiliko yaliyofanywa na Zambia, kwa kuwatoa Joane Benai, Mary Mwakapila na Grace Chanda na nafasi zao kuchukuliwa na Ireen Lungu, Osala Kaleo na Milika Limwanya yalionekana kuisaidia timu hiyo baada ya kupata bao la kusawazisha kwa dakika ya 61 likifungwa kwa penalty na Lungu baada ya beki wa Twiga Stars Fatuma Issa kushika mpira akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mshambuliaji wa She- Polo polo Misoz Chisa Rachel aliifungia timu yake bao la tatu na laushindi dakika ya 90 akitumia vizuri makosa ysaliyofanywa na beki Fatuma Salum aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Anastaz Katunzi bao ambalo liliwapa Zambia matumaini lakini baada ya dakika mbili pambano hilo lilimalizika na Twiga Stars kusonga mbele kufuatia idadi kubwa ya mabao iliyoyapata kwenye mchezo wa awali.
Hiyo ni mara ya pili Twiga Stars kufuzu fainali hizo za Afrika kwa Wanawake mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2011 iliyofanyika Msumbiji na timu hiyo kutolewa kwenye hatua ya makundi ikifungwa na Ghana na baadaye kutoka sare michezo mitatu ikiwemo Afrika kusini.
Post a Comment