Msiba Mzito Tip Top Connection
VILIO na simanzi vilitawala kila kona baada ya tasnia ya muziki nchini kupata pigo, kwa kuondokewa na aliyekuwa mwasisi na meneja wa Kundi la Muziki la Tiptop Connection, Abdul Bonge, aliyefariki dunia ghafla jioni ya Machi 28 akiwa nyumbani kwake Manzese Tiptop.
Abdul Bonge aliyekuwa mwanzilishi wa kundi hilo
imeelezwa kuwa alikuwa mzima wa afya, lakini akapatwa na umauti wa
ghafla akiwa amepumzika nyumbani kwake.
Abdul alifikwa na umauti alipokuwa akikimbizwa
katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kusukumwa na kuanguka,
alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni
Kagera.
Kwa mujibu wa msanii kutoka Tiptop Connection, Ahmad Ally, msiba upo Manzese Tip Top na taratibu za mazishi zinapangwa.
Ally au Madee alisema: “Tangu niingie Tiptop
Connection sikuwahi kutoka na nilikuwa namwambia Bonge kuwa siku yako
haijulikani, leo imejulikana. Nisingekuwa mimi bila yeye, nilijivunia
kuwa naye, nilijiamini popote.
Marehemu atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya
kuwaibua wasanii kama Madee, MB Dogg, PNC, Pingu na Deso, K’ Sher, Z
Anto, Tundaman na wengineo kabla ya kujipumzisha na kumpisha mdogo wake
Babu Tale kuendelea na kazi.
Post a Comment