Lazima awaue tu.. Hii ndio Staili mpya ya Tambwe
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, sasa ni wa kufunga kwa
staili yoyote baada ya juzi Jumapili kufunga bao lake la kwanza kwa mguu
msimu huu lililoingia katika rekodi ya Afrika.
Tambwe ambaye alisajiliwa na Yanga akitokea Simba
Desemba mwaka jana, kabla ya mechi ya jana tayari alikuwa ameifungia
timu hiyo mabao matano katika mashindano ya Ligi Kuu Bara na Kombe la
Shirikisho.
Katika mabao hayo ambayo matatu aliyafunga katika
Ligi Kuu Bara na mawili katika mechi ya awali ya Kombe la Shirikisho,
Mburundi huyo alikuwa ameyafunga yote kwa njia moja ya kichwa.
Wakati juzi akiifungia Yanga bao la tatu dhidi ya
Platinum bao ambalo pia likiwa la tatu kwake katika michuano hiyo,
alionyesha kubadilika akifunga kwa mguu wa kulia akimalizia kazi safi ya
mshambuliaji Mrisho Ngassa.
Bao hilo limemfanya mshambuliaji huyo kufikisha
mabao sita msimu huu na matano kati ya hayo akiyafunga kwa kichwa
akifungana na Ngassa ambaye naye ana mabao matatu katika Kombe la
Shirikisho.
Post a Comment