STRAIKA mpya wa Yanga


 


STRAIKA mpya wa Yanga, Mliberia Kpah Sherman, amesaini mkataba wa miaka miwili klabuni hapo Ijumaa baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyochukuliwa juzi Alhamisi.
  Sherman alisaini jijini Dar es Salaam mbele ya Mwen yekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Isack Chanji, huku akiahidi kujituma akisema amefurahi kukuta mazingira mazuri Yanga.
Huku Yanga ikipiga bao hilo, pia imeipiku Simba kwenye ukusanyaji wa mapato ya michezo saba ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ingawa Simba imeongoza kwa kuangaliwa na mashabiki wengi uwanjani.
Takwimu pia zinaonesha Simba imepata hasara kubwa ya mapato kuliko Yanga ukilinganisha msimu uliopita kipindi kama hiki.
Takwimu za Bodi ya Ligi ya Tanzania (TPLB) zinaonyesha Yanga ndiyo klabu ya Ligi Kuu inayojikusanyia mapato mengi zaidi mpaka sasa kwani imeingiza Sh193,323,948 (mara 22 ya mapato ya Azam kwenye michezo saba) wakati Simba imeingiza Sh 153,027,754.
Kwa upande wa watamazaji, Simba imeongoza kwa kushuhudiwa na mashabiki 54,772 wakati Yanga imetazamwa na mashabiki 54,284 tangu ligi ya msimu huu ianze.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Azam FC ambayo ni klabu tajiri zaidi nchini, haijakusanya mapato makubwa wala michezo yake haijawavuta mashabiki wengi. Imezidiwa pia na Mtibwa, Coastal, Prisons, Mbeya City na JKT Ruvu.
Kwenye michezo saba, Azam imeingiza Sh8,630,108 tu na imeshuhudiwa na mashabiki 8,650. Kagera Sugar ndiyo imekusanya kiduchu.
Makadirio yanaonyesha Simba imepata hasara ya Sh81 milioni kwani msimu uliopita katika kipindi kama hiki ilipata Sh 234 milioni. Yanga imepata hasara ya Sh 9 milioni.

No comments