Neiva alisema: “Kuna wachezaji wengi Yanga, tena wenye uwezo wa hali ya juu, lakini linapokuja suala la uchezaji wanatofautiana kwenye mambo mengi.
“Tazama mazoezi ya jana (juzi Jumanne) tuliamua kuwapa mazoezi wachezaji kwa kuchezesha vikosi viwili tofauti kwa lengo la kupima uwezo wa mabeki kuzuia mashambulizi na vilevile kupima makali ya washambuliaji wanapovaana na mabeki.
“Tuligundua kuwa endapo safu ya ushambuliaji ya mbele itakapokuwa na wachezaji; Ngassa, Msuva na Kiiza timu inaweza kufaidi kwa kufunga magoli na kuzipa tabu safu za ulinzi zisizo na umakini.
“Tena kuna mtu kama Hussein Javu mwenye kasi kama hiyo ingawa anatofautiana na Tegete ambaye ni mmaliziaji na si mkimbiaji kwa kasi anapokuwa na mpira.”
Msimu uliopita kwenye mzunguko wa pili, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Van Pluijm alikuwa akiwatumia wachezaji hao watatu kwenye safu ya ushambuliaji huku mbadala wao akiwa ni Javu.
Post a Comment