Yanga mbioni kumnasa Mwadini Ali

Yanga mbioni kumnasa Mwadini Ali
Mkataba wa Mwadini unamalizika Oktoba 2015 na kipa huyo amesema miaka minne aliyoichezea timu hiyo akitokea Mafunzo ya Zanzibar inatosha na anataka kusaka changamoto mpya

KLABU ya Yanga ipo mbioni kumsajili kipa chaguo la kwanza wa Azam FC Mwadini Ali kwa dau la Sh. Milioni 60 katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
Viongozi wa kamati ya usajiliwa wa klabu ya Yanga bado wapo katika mazungumzo na kipa huyo wakimshawishi kujiunga na mabingwa hao wa zmani ili kuziba nafasi ya Juma Kaseja anayesemekana kutaka kujiunga na timu yake ya zamani Simba.
Mwadini Ali ameongea na Goal na kukiri kuzungumza na viongozi wa Yanga na kusema endapo ataridhika na maslahi atakuwa tayari kujiunga na timu hiyo yenye upinzani mkubwa ya timu yake ya sasa Azam FC..
Mkataba wa Mwadini unamalizika Oktoba 2015 na kipa huyo amesema miaka minne aliyoichezea timu hiyo akitokea Mafunzo ya Zanzibar inatosha na anataka kusaka changamoto mpya

No comments