Utata juu ya Jackie Appiah, John Dumelo sasa wafika tamati
John Dumelo na Jackie Appiah walichaguliwa kutoa hamasa kwa wananchi kuisapoti timu yao kwenye mashindano hayo. Baada ya timu yao kutolewa, mashabiki wa soka walikuja juu na kusema kuwa mastaa hao wamelipwa kiasi kikubwa cha pesa tofauti na kazi yao.
ULE uvumi ulikuwa umeenea kuwa mastaa wa filamu wa Ghana, Jack Appiah na John Dumelo wamefuja pesa za serikali, kwenye kampeni za Kombe la Dunia kwa timu yao ya Ghana umekwisha baada yavyombo vya sheria kufuatilia na kuweka wazi kila kilichojiri.
John Dumelo na Jackie Appiah walichaguliwa kutoa hamasa kwa wananchi kuisapoti timu yao kwenye mashindano hayo. Baada ya timu yao kutolewa, mashabiki wa soka walikuja juu na kusema kuwa mastaa hao wamelipwa kiasi kikubwa cha pesa tofauti na kazi yao.
Kilichowakera zaidi Waghana ni pale waliposhuhudia wawili hao wakipanda ndege kwenda kuisapoti timu yao ilipokuwa ikicheza kwenye mashindano hayo.
Kwa mujibu wa Mtandao wa africannews baada ya kufanyika kwa uchunguzi, iligundulika kuwa wawili hao walifanya hamasa hizo kwa kutumia pesa zao.
Post a Comment