MARRIED BUT NOT ENGAGED

Hivi unajua maana ya neno “engagement?” yaani kile kitendo cha mwanaume kutangaza mbele ya umma jinsi moyo wake ulivyompenda binti fulani na kama alama ya kuthibitisha nia hii ya dhati kijana huyu anachukua pete na mumvika binti huyu.

Kama ni kwa wenzetu wazungu basi kijana atapiga goti na kumuuliza mwanadada “will you marry me?” Mara baada ya tendo hili hakuna kijana yeyote anayeweza kuja kutangaza kumpenda binti huyu, na kinachofuta hapo ni mipango ya ndoa.

Neno “engagement” linatokana na neno “engage”, neno “engage” humaanisha kuchukua nafasi “to occupy”, kujihusisha kwa dhati au kuamua kuhusiana kwa dhati “to involve” au pia “to absorb”.

Maneno haya yote ya kiingereza yanamaanisha kwamba mara kijana anapoamua kum “engage” mpenzi wake wakike wote wawili wame kubali kumilikiana, kila mmoja kushukua nafasi kubwa kwenye moyo wa mwenzake, kila mmoja kuumeza moyo wa mwenzake kwa penzi, na pia kila mmoja kuamua kwa dhati kujihusisha vilivyo katika maisha ya mwenzake.

Sasa kama hizi ndizo maana za kile kitendo ulichomfanyia mke wako miaka hiyo ya nyuma au kama hii ndiyo maana ya kile ulichofanyiwa na mumeo siku zile akikuchumbia, nikuulize, je maana ile ya “engagement” bado ni halisi hadi leo???? Au iliishia siku ile ile ya “engagement?” au yamkini ulivikwa tu pete na ukafurahia pete ambayo ni alama tu wakati kamwe hujawahi kuuona upendo ambao pete hiyo iliumaanisha?

Na je, kwa kutazama maana hizi nilizozitoa, ukiangalia mahusiano yenu unaona ile “engagement” bado ipo??? Au ilishakufa??? Au haijawahi kuwapo?? Kama jibu ni ilishakufa au haijawahi kuwapo basi hiyo pete ya “engagement” kidoleni kwako ni mzigo tu, kwanza unaweza kukuta hata aliye ku “engage” haishi na wewe tena, ana wengine, sasa hiyo alama inamuwakilisha nani hapo kidoleni?

Kama unapete ya “engagement” kidoleni jiulize, Je hii ni alama ya ushuhuda wa penzi halisi katika mahusiano yetu? Au ni alama ya kihistoria inayoonyesha kitu ambacho hakipo tena? Kama ni alama ya kihistoria basi haistahili kuwa kidoleni bali kwenye nyumba ya makumbusho “take it to museums”