Mkurugenzi mkuu wa ”Merumba Group”alikuwa ofisini kwake akimsimulia binamu yake Richard mkasa uliomkuta miaka miwili iliyopita. “Kuna mdada mrembo sana alikuja ofisini kwangu hapa na kuniambia.” “Samahani bosi.” “Bila samahani nikusaidie nini?” “Naomba unisaidie kupata ajira.” “Ajira gani?” “Nikupikie ,nikufulie,nikunyooshee nguo,nikufagilie nyumba,nikuoshee vyombo,nikutandikie kitanda,nikuogeshe na kadhalika.” “Ehee makubwa!Si useme unataka kuwa mke wangu ,naona kazi zote ulizozitaja zinafanyika nyumbani na hapa ni ofisini kulikoni?” Yule mrembo kilio kikamtoka kikiambatana na machozi na kutamka :–
“Siyo mimi ndo nataka kuwa hivyo ila ni maisha ndiyo yanataka hivyo.Nilimaliza chuo kikuu Mzumbe mwaka 2005 na kutunukiwa shahada ya kwanza ya utawala/uongozi wa biashara nikiwa mwanachuo bora niliyepata alama za juu kuliko wanachuo wote katika “faculty of commerce” kwa mwaka huo.
Kutokana na matokeo yangu kuwa juu mno kwa kupata “gpa” ya 4.8, chuo kilinitafutia kazi katika benki ya biashara ya kimataifa inayofanya shughuli zake hapa nchini.Baada ya kukamilisha taratibu zote za usaili na kuajiriwa rasmi,siku ya kwanza ambayo natakiwa kuanza kazi niligongwa na gari nikiwa navuka barabara kuelekea ndani ya jingo la hiyo benki.
Aliyenigonga akakimbia,wasamalia wema wakaniokota na kunipeleka hospitali.Nilipooza nusu mwili kutokana na mshituko nilioupata kwa kulala kitandani kwa muda wa miaka mitano.
Baba aliuza kila kitu ili aweze kunitibu ,mwishowe akaingia kwenye madeni na kuukumiwa kwenda jera kwa kushindwa kulipa deni la shilingi milioni hamsini kwa ajili ya matibabu yangu nchini India.
Mama alipandwa na shinikizo la damu siku ambayo baba aliukumiwa kwenda jera miaka kumi na mitano na kufariki pale pale mahakamani.
Baba akiwa gerezani baada ya miaka miwili alifariki kutokana na kuugua ugonjwa wa moyo uliosababishwa na msongo mwingi wa mawazo juu yangu na hatima yake gerezani,kazi ngumu alizokuwa akifanyishwa,mlo duni waliokuwa wanapewa wafungwa pamoja na mazingira machafu ya gereza.
Benki ile ambayo nilitakiwa nianze kufanya kazi hawakutoa msaada wowote kwa kigezo kuwa bado nilikuwa sijaanza kiufanyia kazi.
Baada ya kurudishwa hospitalini Muhimbili kwa msaada wa ubalozi wa Tanzania nchini India kutokana na fedha za matibabu kuisha ambazo baba alikopa na ugonjwa wangu kushindikana kutibika na baba na mama wameshafiriki,hospitalini hapo nilibaki mimi peke yangu kwa maana hata ndugu nao walinikimbia.
Ikabidi watafutwe watawa wanichukue kwa ajili ya kuniuguza. Siku moja usiku wa saa tisa baada ya miak mitano tokea siku ile niliyopata ajali, mvua kubwa ilikuwa inanyesha ikiambatana na radi na ngurumo za kutisha ,muda huo nilikuwa macho wazi, niliona kama mwanga wa tochi umepenya katika bati na kunimulika usoni.
Ghafla mwili wangu ukaanza kutetemeka kama mtu mwenye kifafa na kupoteza fahamu. Nilikuja kushituka saa kumi na moja alfajili na kujiona mwili ni mwepesi na nilipojaribu kuinuka nikajikuta nainuka,ahah nikajishangaa nikajikuta napiga kelele mama aha ,watawa waliokuwa katika misa ya alfajili wakaja na waliponiona na wao wakashangaa.
Baada ya miaka miwili mwili kuwa sawa nikaamua nirejee uraiani kutafuta maisha.Sikuwa na pa kwenda kwa maana vitu vyote baba aliuza ila nilimwomba mungu aniongoze niende mahali salama.
Nikiwa natembea tembea barabarani usiku nilikutana na dada mmoja na kumweleza shida yangu akakubali kunisaidia na akaniambia yeye anauza baa na sharti nikitaka kukaa kwake nami niuze baa.
Sikuwa na na jinsi ikanibidi nikubaliane nae.Nikawa nauza baa, meneja anataka nivae nguo fupi mapaja yawe wazi na nguo ya juu iwe inaacha sehemu kubwa ya matiti nje.
Usiku wanaume walevi wananitongoza nikafanye nao ngono kwani tayari wameshamlipa meneja ,nikakataa.Wanaume wale walienda kumfokea meneja .”We meneja mbona Malaya wako hataki kwenda kutuburudisha?Hajui kama tumeshakupa fedha kwa ajili yake ?Turudishie fedha zetu .”
Meneja alinitaka niende kufanya ngono na wale wanaume ,nikamkatalia na kumwambia “Mimi sijiuzi bali ninafanya kazi ya kuwaudumia wateja vinywaji .”Meneja alikasirika sana na kuniambia kama sitaki basi na mimi kazi sina.Akanifukuza kama mbwa mdowezi huku akinikashifu .”Mwanamke gani wewe hutaki kuwastaheresha wanaume?
Hujui kuwa kazi ya mwanamke hapa duniani ni kuwaliwaza wanaume kingono?Pumbavu kabisa toka hapa .” Nilitoka pale huku nalia nikarejea kwa yule dada muuza baa siku hiyo alikuwa mapumzikoni,hata kabla sijakaa akaniambia.”Eheee bibi,meneja kanipigia simu na kunieleza yote uliyoyafanya na mimi sikutaki tena uishi humu ndani,unazani mimi ninaishije hapa mjini ?Mimi ninafanya kazi kama hiyo meneja aliyokuambia wewe hutaki,unazani nani atakulisha na kukulaza bure?
Embu toka ndani mwangu mpumbavu wewe ,hapa ni mjini ukitaka kula vya watu na wewe lazima uliwe hata Raisi wako anasemaga, kwenda huko ukafie mbali alah umeniuzi kama nimekufumania na buzi langu kenge wewe.
Nililia sana siku ile, dunia niliiona chungu sikutamani hata kuendelea kuishi lakini kama kuna mtu alikuwa ananiambia moyoni “Kama sikuweza kufa katika ile ajali na kulala kitandani miaka mitano basi sitaweza kufa mpaka muda wangu wa kuishi hapa duniani utakapo kwisha.”
Siku hiyo nililala sokoni ambalo lipo maeneo hayo.Maisha yangi yakawa hapo sokoni nikiwa na akina dada wengine ambao nao hawana sehemu ya kulala tukiwa tunafanya kazi ya kubeba matenga yaliyoletwa na malori kutoka mikoani.
Baada ya mwaka mmoja nikiwa pale sokoni kuna mdada mmoja alikuwa ananunua tenga la nyanya na muuzaji aliniita ili nilibebe na kulipeleka kwenye gari la huyo mdada.Ahaah, yule mdada alishituka na kunifanya na mimi nimuangalie kwa umakini na kumtambua ni rafiki yangu tulisoma wote shule ya sekondari Jangwani.
Tulikumbatiana na kuanza kulia,alishangaa mno kuniona niko vile ndipo nikamueleza kila kitu kilichonitokea,alilia sana na kunichukua mpaka kwake anapoishi na mumewe na muda huo alikuwa safarini kibiashara nchini Ufaransa na angerudi baada ya miezi sita.
Mimi na rafiki yangu huyo tulianza kufuatilia vyeti vyangu vipya kuanzia sekondari mpaka chuo na kufanikiwa kuvipata na kuanza kuomba kazi sehemu mbalimbali na nilipoitwa kwa ajili ya “interview” niliishia kuombwa rushwa ya ngono nikakataa na kazi nikanyimwa ingawaje nilikuwa napata alama za juu kuliko waombaji wote katika kila interview niliyokuwa nakwenda kuifanya.
Rafiki yangu alipata safari ya kwenda nchini Malaysia kibiashara na baada ya hapo aliunganisha safari kwenda Ufaransa kwa mumewe ila ndege aliyopanda ilidondoka baharini na kupotelea huko.
Pale kwake nilibaki mimi na kodi ya nyumba ilipoisha,mwenye nyumba akanifukuza kwani walikuwa wamepanga nikarudi tena mitaani kupambana na maisha.
Baada ya miaka miwili ya mateso na misukosuko mingi nilibahatika kupata kibarua cha kubeba zege hapa Posta Katika ghorofa jipya linalojengwa na kuweza kupanga chumba kimoja maeneo ya Mbagala.
Na jana wakati narudi nyumbani kutoka kibaruani ndo nikaliona bango la ofisi yako kule chini limeandikwa “MERUMBA GROUP”.Kuna kitu moyoni kikaniambia nichukue vyeti vyangu na kuja kujaribu kuomba kazi hapa.
Lakini nikajiambia kila ninapokwenda kuomba kazi naishia kuombwa rushwa ya ngono na nikikataa nanyimwa kazi basi nikajisemea nikifika hapa niombe kazi zinazofanyika nyumbani.”Alimaliza kusimulia yule mrembo huku akilia na machozi yakimtoka.
“Daah aise Richie nililia sana alivyonisimulia vile kwa maana yule mdada mimi ndiye niliyemgonga ,alafu yule rafiki yake aliyeanguka na ndege alikuwa ni mke wangu kama unakumbuka vizuri mke wangu alikufa katika ajali ya ndege miaka mingi imepita.Na nilipopata taarifa ya ajali ile nilizimia kwa muda wa mwaka mmoja na namshukuru mungu wazazi wangu walinitibu mpaka nikapona.
Alinishangaa kwa nini nami nalia vile nikamweleza kila kitu kilichotokea ,tulikumbatiana na kubaki tunalia wote. Nikamwomba msamaha kwa kumgonga na gari na kukimbia na kumsababishia matatizo makubwa ila mungu aliacha jambo hilo litokee kwa makusudi maalum na yeye akanisamehe.
Nilimchukua kutoka pale ofisini na kumpeleka moja kwa moja kwa wazazi wangu na kuwaeleza kila kitu nao wakawa wanalia.Mwezi mmoja nikafunga nae ndoa maana kusema ukweli ni mrembo sana ingawa matatizo yaliuficha urembo wake na alikuwa hajaguswa kabisa waswahili wanaita kigori yaani bikra.
Nakumbuka hata wewe ulipokuwa nchini Japani ulishangaa kwa nini naoa ghafla bila ya kutoa taarifa mapema na wewe kushindwa kuuzulia harusi yangu ni kutokana na kutaka kuondoa machungu aliyokuwa nayo na mimi pia.
Sasa hivi nimpatia kazi kama mkurugenzi mkuu msaidizi akisimamia makampuni na biashara zangu zote ninazomiliki na yupo nyumbani ana mimba ya miezi tisa kasoro siku chache ajifungue niitwe na mimi baba teh teh teh.
Dah nilimsababishia mateso mke wangu na kweli maisha hayatabiriki lakini mungu ni mwema sana kwetu sisi binadamu.
Post a Comment