Kiungo Coutinho bila wasi ajihalalisha namba Yanga


 KOCHA wa soka ambaye pia ni na mchambuzi wa mchezo huo, Joseph Kanakamfumu, anaamini kwamba kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho, hana uwezo wa kumzidi Haruna Niyonzima ambaye hachezeshwi dakika 90.

 Lakini Coutinho ambaye yupo kwao likizo kwa sasa ameanza mazoezi ya Gym nchini humo ili kujiweka fiti kwaajili ya mechi zilizosalia za Ligi Kuu Bara msimu huu.
Coutinho amesajiliwa na Yanga msimu huu na kufanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kinachofundishwa na Mbrazili mwenzake Marcio Maximo.
Akizungumza kutoka kwao Brazili walikokwenda kwa mapumziko ya siku 10 pamoja na Maximo na straika Genilson Santos ‘Jaja’, Coutinho alisema ameamua kuanza kufanya mazoezi hayo kujiweka fiti ili aweze kuisaidia Yanga zaidi.
“Nimeanza mazoezi ya Gym huku Brazili, nataka kujiweka fiti ili nikirudi niweze kuisaidia Yanga zaidi,” alisema Coutinho kwa ufupi alipowasiliana na Mwanaspoti. Awali kiungo huyo alisema amepanga pia kuutumia muda huo kufanya mazoezi binafsi ya kupiga mipira ya faulo pamoja na kuongeza mbinu za uwanjani ili aweze kufanya vizuri zaidi atakaporejea.
Coutinho na Jaja wameingia lawamani kwenye kikosi cha Yanga kwa kushindwa kucheza kwa kiwango cha juu tofauti na ilivyotarajiwa na mashabiki.

No comments