Wanajeshi kumi na wawili nchini Nigeria wamepewa adhabu ya kifo kwa uasi pamoja na jaribio la mauji.Hii
ni baada ya kumfyatuliwa bunduki afisa mkuu anayeongoza operesheni ya
kupambana dhidi ya kundi haramu la kiislamu la Boko Haram kati mji wa
Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi, mwezi wa Mei.
Wanajeshi wengine watano waliachiliwa baada ya ushahidi kukosekana.
Wanajeshi hao 12 walipatikana na hatia ya kumfyatulia risasi Jemedari amadu Mohammed.
Wanajeshi hao walikasirishwa na kamanda wao ambaye walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao kushambuliwa.
Jeshi
la Nigeria limeshindwa kuwashinda Boko Haram na wanajeshi wamekuwa
wakilalamika kuwa kila wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram
hawana silaha za kutosha kukabiliana nao.
Wote walikana mashtaka hayo katika Mahakama ya kijeshi mjini Abuja.
Kitengo hicho cha Jeshi ndicho kinakabiliana na Boko Haram
Mahakama ya kijeshi ya watu
tisa ilisikiza kuwa tukio hilo lilitendeka baada ya kufyatuliwa kwa
risasi kwa afisa mkuu wa kitengocha 7 cha jeshi la Nigeria.
Ilimbidi Generali Amadu Mohammed kujificha walipomlenga na bunduki zao.
Hata hivyo, hakuumia.
Kiongozi
wa mahakama Chukwuemeka Okonkwoalisema kuwa hata kama hukumu hizi
zilikuwa chini ya udhibitisho wa mamlaka ya jeshi la Nigeria, hakukuwa
na shaka juu ya uzito wa kosa hilo.
Mwezi uliyopita, kundi la
wanajeshi kaskazini masharikimwa Nigeria walikataa kupambana na Boko
Haram mpaka wapatiwe vifaa bora, mmoja wao aliiambia BBC.
Post a Comment