Mateka mwengine akatwa kichwa na IS


Serikali ya Uingereza imesema kuwa inachukua
hatua za dharura ili kubaini ukweli wa kanda ya
video inayoonyesha mateka wa Uingereza David
Haines aliyetekwa nyara na kundi la himaya ya
kiislamu akikatwa kichwa.
Mfanyikazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini
Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana
ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa,
kando yake akiwa ni mtu aliyeficha uso wake
ambaye amebeba kisu.
Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa
kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu
anaonekana akishtumu mataifa yanayounga
mkono Marekani,naye Haines ambaye
anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana
akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David
Cameron kwa hatma yake.
Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa
Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.
David Cameron
Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza
David Cameron ameshtumu kukatwa kichwa kwa
David Haines kama kitendo cha kishetani.
Amesema kuwa wauaji watakamatwa na
kuchukuliwa hatua za kisheria ata iwapo
itachukua mda mrefu.
Katika taarifa yake rais Obama pia ameshtumu
mauaji ya kikatili ya David Haines.
Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza
kifo cha mateka huyo na kungezea kuwa
itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa
ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu
tishio hilo kwa ulimwengu.
Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley
waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita.

No comments