FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA

Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya
Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo ( Chadema) Taifa baada ya
kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani
wake Ngambaranyela Mongatero akipata
kura 20.
Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika
uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara
imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari
aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za
hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea
asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa
Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku
mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph
akiambulia kura 163.

No comments