MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI
Bw.
Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa
wanafunzi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013
Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.
Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto
pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo
cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda
kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho
kinamilikiwa na Bw.
Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa
miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania
mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo
pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee
tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza
umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya
kilimo Tanzania.
Dorice Mollel amesema “ hichi ni kitu
cha muhimu sana nikiwa kama mrembo nikirudi nyumbani na kuieleza jamii
inayonizunguka ili kutuletee faida baadae nchini kwetu”.
Post a Comment