Jinsi Arsenal ilivyoisambaratisha Man City
Timu ya Arsenal imeichabanga timu ya man ciity Bao 2 bila majibu katika
mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa kwenye Dimba la Etihad.Arsenal
ambao walikua na kasumba mbaya kila wakutanapo na timu kubwa walivunja mzizi wa fitina angali wakicheza kwenye kiwanja cha ugenini.Shukrani zimuendee Santiago Cazorla aliyefunga bao la kwanza dakika ya 24 kwa mkwaju wa penati baada ya Kompony kumuangusha beki Monreal.Cazorla alitengeneza tena bao la pili la Arsenal lililofungwa na Olivier Giroud.Ushindi huo umerejesha imani na matumaini kwa washabiki wa Arsenal kurudi kwenye timu 4 za juu
Post a Comment